POLISI WAKANUSHA MADAI YA MTU KUPIGWA RISASI NYAHURURU
Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS) imekanusha madai kwamba mtu alipigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea katika mkutano wa kisiasa mjini Nyahururu.
Polisi wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kundi la watu lilivuruga mkutano huo kwa kurusha mawe, na kusababisha baadhi ya watu kupata majeraha madogo, lakini hakuna tukio la ufyatuaji risasi lililoripotiwa.
Kauli hiyo imejiri baada ya Gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata kudai kuwa dereva wake, Joseph Gitau, alipigwa risasi na anaendelea kupokea matibabu hospitalini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

