MILLIE ODHIAMBO ALENGA URAIS MWAKA 2032
Mbunge wa Suba Kaskazini, Millie Odhiambo, amepuuzilia mbali wito wa kuwania ugavana wa Homa Bay, akisema uongozi wa kaunti si sehemu ya wito wake wa kisiasa, huku akisisitiza azma yake ya kuwania urais wa Kenya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2032.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja nchini, Odhiambo amesema hana nia ya kuingia katika kinyang’anyiro cha ugavana na badala yake anaangazia safari yake ya muda mrefu ya kuwania urais.
Mbunge huyo pia amesisitiza kuwa atazungumzia waziwazi masuala ya utawala na kukosoa mapungufu ya uongozi bila kujali misimamo ya kisiasa au miungano anayohusishwa nayo, ikiwemo chama cha ODM.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

