UHISPANIA YATINGA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA
Uhispania imefuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa 2-0 Ufaransa katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jijini Dallas Marekani.
Kikosi cha kocha Luis de la Fuente kilitawala mchezo na kujihakikishia ushindi kupitia mabao ya Mikel Oyarzabal, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, na Pedro Porro.
Kwa ushindi huo, Uhispania itasafiri kuelekea New Jersey kusubiri mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya England na Argentina, ikisaka kutwaa taji la Kombe la Dunia kwa mara ya pili katika historia yake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

