RUTO KUTOA HOTUBA YA HALI YA TAIFA LEO
Rais William Ruto anatarajiwa kutoa hotuba ya Hali ya Taifa leo mbele ya kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti katika majengo ya Bunge jijini Nairobi.
Rais atatumia hotuba hiyo kueleza hatua zilizopigwa na serikali yake, mafanikio yaliyopatikana pamoja na vipaumbele vya utawala wake.
Hotuba hiyo ya kila mwaka humpa rais nafasi ya kuwafahamisha Wakenya kuhusu utekelezaji wa sera na mipango ya serikali, pamoja na hatua za nchi katika kutimiza wajibu wake wa kikatiba.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

