RUTO AAHIDI KUPUNGUZA GHARAMA YA MAISHA
Rais William Ruto amehitimisha ziara ya kikazi ya siku nne katika eneo la Gusii, akisisitiza dhamira ya serikali yake kupunguza gharama ya maisha na kuboresha hali ya kiuchumi kwa Wakenya.
Ruto amesema serikali inalenga kuwawezesha wananchi kubaki na fedha zaidi za matumizi, huku ikiendeleza miradi ya miundombinu na maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika ziara hiyo, Rais alitembelea miradi inayoendelea na kufanya mikutano na viongozi pamoja na wakazi wa eneo hilo
.Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

