KOCHA MUMO AONYA KUHUSU VIWANGO VIGUMU VYA OLIMPIKI 2028
Kocha wa mbio za kasi wa Jeshi la Kenya KDF, Vincent Mumo, ameeleza wasiwasi kuhusu viwango vigumu vya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028 jijini Los Angeles, akitaka maandalizi yaanze mapema.
Mumo amependekeza kuanzishwa kwa kambi za mazoezi ili kuwasaidia wanariadha kufikia viwango hivyo, vilivyotangazwa na Shirikisho la Riadha Duniani na ambavyo ni vigumu zaidi ikilinganishwa na vile vya Olimpiki ya Paris 2024.
Katika mbio za mita 100, wanaume wanahitajika kutumia sekunde 9.93 na wanawake 10.96, huku Mumo akionya kuwa wanariadha watalazimika kuboresha sana muda wao ili kupata tiketi ya mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

