Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

EMERGING STARS YAICHAPA IVORY COAST 2-1

Timu ya Kenya Emerging Stars imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ivory Coast katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 23, iliyochezwa katika uwanja wa Nyayo.

Henry Omollo alivunja kimya kwa kuifungia Kenya bao la kwanza dakika ya 64, akimalizia pasi ya Lawrence Okoth, kabla ya Andreas Odhiambo kuongeza la pili dakika ya 83 baada ya kupenya safu ya ulinzi ya wapinzani.

Kocha Anthony Kimani amewapongeza wachezaji wake kwa kutokata tamaa licha ya kushinikizwa, huku ushindi huo ukiipa Kenya faida kuelekea mechi ya marudiano itakayochezwa Jumanne mjini Abidjan.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *