KENYA YATWAA UBINGWA WA NDONDI AFRIKA
Timu ya ndondi ya Kenya, Hit Squad, imetawazwa bingwa wa jumla katika Mashindano ya Ndondi Afrika 2026 yaliyokamilika katika Ukumbi wa Kasarani Indoor Arena, baada ya kutwaa medali 15, zikiwemo dhahabu tano, fedha tatu na shaba saba.
Grace Atieno, Rosemarion Otieno, Juliet Opondo, Kelvin Maina na Friza Asiko ni miongoni mwa mabondia walioipa Kenya dhahabu, huku Veronica Mbithe akijinyakulia medali ya fedha baada ya kupambana na Fatiha Mansouri wa Algeria.
Kenya ilimaliza kileleni kwa jumla ya medali 15, mbele ya Algeria iliyopata medali 11, zikiwemo dhahabu tano, huku Uganda ikishika nafasi ya tatu kwa medali 11, ikiwemo dhahabu nne.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

