WANAFUNZI UoN WAPANGA MAANDAMANO HADI IJUMAA
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wanapanga kuandamana kila siku hadi Ijumaa wakiongeza shinikizo kwa serikali na wahadhiri kutatua mgomo ambao umesitisha masomo katika vyuo vikuu vya umma kwa karibu mwezi mmoja.
Wanafunzi hao wanataka suluhu ya haraka ya mzozo kati ya wahadhiri na serikali, wakisema kucheleweshwa kwa masomo kunaathiri mitihani yao, maendeleo ya kitaaluma na mipango ya kuhitimu.
Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Ojwang Obunde, amesema maandamano yataendelea wiki nzima hadi shughuli za masomo zitakaporejea katika hali ya kawaida.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
