MAANDAMANO YA SABA SABA YA AMANI: WASEMA WANAHARAKATI
Kenya inapojiandaa kuadhimisha siku ya saba saba kesho juma nne baadhi ya wanaharakati wakiongozwa na kundi la Grassroots economic justice movement wamewasilisha notisi rasmi kwa inspekta mkuu wa polisi Daglas Kanja, kamanda wa polisi wa Nairobi na mkuu wa kituo cha polisi cha Nairobi Central kuhusu maandamano yaliyopangwa kufanyika jijini Nairobi.
Kundi hilo limesema maandamano hayo yatakuwa ya amani na yatashirikisha mamia ya wananchi watakao andamana kutoka bustani la Jivangee hadi majengo ya bunge kabla ya kuwasilisha maombi mbali mbali, yakiwemo kukomesha mauaji kiholela, visa vya kutoweka kwa lazima na matumizi ya nguvu kupita kiasi miongoni mwa maafisa wa polisi.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

