Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

EMERGING STARS YALENGA KUMALIZA KAZI ABIDJAN

Kocha wa Kenya Emerging Stars, Anthony Kimani, ana imani kikosi chake kina uwezo wa kuishinda Ivory Coast katika mechi ya marudiano mjini Abidjan na kusonga karibu na kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 23 mwaka 2027.

Kenya inaingia katika mechi hiyo ikiwa na faida ya mabao 2-1 kutoka mchezo wa kwanza jijini Nairobi, ambapo Henry Omollo na Andreas Odhiambo walifunga mabao ya ushindi kipindi cha pili baada ya kuingia kama wachezaji wa akiba.

Kimani amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na Ivory Coast kuwa nyumbani, lakini anataka wachezaji wake kudumisha ari ya kupambana na makali ya ushambuliaji ili kulinda ushindi wao na kusonga mbele.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *