Tuesday, October 6, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RUTO ATETEA HAZINA YA MIUNDOMBINU

Rais William Ruto ametetea kuanzishwa kwa Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu (NIF) akisema itasaidia kufadhili miradi ya maendeleo bila kuongeza deni la taifa.

Akizungumza Kaunti ya Embu, Rais amesema hazina hiyo tayari imekusanya shilingi bilioni 350 kupitia mauzo ya baadhi ya mali za serikali, ikiwemo hisa za Kenya Pipeline Company na sehemu ya hisa za Safaricom.

Ruto amesema fedha hizo zitasaidia kuharakisha maendeleo ya miundombinu na kushughulikia pengo la maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *