Tuesday, November 24, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

NDORO NA MWANGI WALENGA DHABABU MAREKANI

Wakimbiaji na wanamichezo wazoefu wa Kenya, Millicent Ndoro na Peter Mwangi, wanalenga kutwaa medali za dhahabu katika Mashindano ya Dunia ya Riadha za Ndani kwa Wanamichezo Wakongwe yatakayofanyika Gainesville, Florida, Marekani, baada ya kufanya vizuri katika mchujo wa kitaifa.

Ndoro mwenye umri wa miaka 40 alishinda mbio za mita 60 na 200 katika kitengo cha wanawake wenye umri wa miaka 40, akitumia sekunde 7.57 na 24.2 mtawalia, na sasa analenga kutwaa dhahabu katika mbio zote mbili kama alivyofanya mwaka 2025.

Kwa upande wake, Mwangi alishinda kurusha tufe katika kitengo cha wanaume wenye umri wa miaka 45 kwa umbali wa mita 15.85, na analenga kutetea taji lake baada ya kutwaa dhahabu katika mashindano ya mwaka jana kwa kurusha mita 14.79.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *