Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

SIFUNA AUNGANISHA UFISADI NA HASIRA ZA WANANCHI

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amesema ufisadi unaoongezeka nchini ni miongoni mwa sababu kuu zinazochochea hasira za wananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Sifuna amesema alifanya mazungumzo na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akitaka kujua chanzo cha kuongezeka kwa malalamishi ya Wakenya, ambapo Gachagua alitaja ufisadi kuwa miongoni mwa sababu kuu za wananchi kutoridhika.

Sifuna amesisitiza kuwa kiwango cha ufisadi nchini kimefikia hali isiyoweza kuendelea kuvumilika, huku akihusisha malalamishi hayo na wito wa baadhi ya wananchi wa kutaka Rais William Ruto kuondoka madarakani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *