Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

EACC YAONYA KUHUSU UPENDELEO KATIKA AJIRA ZA KAUNTI

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC, imeibua wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ufisadi na ukiukaji wa maadili katika usimamizi wa rasilimali watu katika serikali za kaunti.

Tume hiyo imesema baadhi ya serikali za kaunti zinadhoofisha bodi za utumishi wa umma na kukiuka kanuni za ajira, huku nafasi za kazi zikidaiwa kutolewa kwa washirika wa kisiasa, wanaotoa hongo na jamaa za viongozi badala ya watahiniwa wenye sifa.

Katika hotuba iliyowasilishwa na meneja wa EACC eneo la Magharibi, Eric Gumbi, tume hiyo imeonya kuwa bodi hizo zinaingiliwa kisiasa na kuwataka magavana na viongozi wengine kuheshimu uhuru wake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *