MARAGA NA KARUA WATAKA UPINZANI KUUNGANA
Viongozi wa upinzani wameongeza juhudi za kuimarisha umoja wao kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, wakisisitiza umuhimu wa kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika kinyang’anyiro dhidi ya Rais William Ruto.
Wakizungumza mjini Kitale kaunti ya Trans Nzoia, aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga na kiongozi wa PLP Martha Karua wamepuuzilia mbali madai ya kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa ndani ya upinzani.
Viongozi wameikosoa serikali ya Kenya Kwanza kwa kile walichokitaja kuwa kuzorota kwa uongozi, kuongezeka kwa ufisadi na kudorora kwa huduma za afya ya umma.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

