GACHAGUA AMTAJA RAYMOND OMOLLO KAMA KIONGOZI HALISI WA MDG
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amedai kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, ndiye kiongozi halisi wa chama cha MDG na anamsaidia Rais William Ruto kuwaondoa kisiasa viongozi waliokuwa washirika wa marehemu Raila Odinga.
Gachagua anadai Omollo anaratibu mtandao unaolenga kuwashinda wabunge, maseneta na magavana katika uchaguzi wa 2027, huku wabunge 29 wakitajwa kuwa miongoni mwa wanaolengwa.
Katika mahojiano, Gachagua pia alidai kuwa maafisa wakuu serikalini na katika mashirika ya umma watajiuzulu kabla ya Februari 10, 2027, ili kuwania nyadhifa za kisiasa chini ya mpango huo unaodaiwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

