Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

OBURU ASISITIZA ODM BADO INA NGUVU NYANZA

Kiongozi wa ODM, Dkt Oburu Odinga, amepuuzilia mbali kuimarika kwa chama cha MDG katika eneo la Nyanza, akisisitiza kuwa ODM bado ndicho chama chenye ushawishi mkubwa eneo hilo.

Oburu aliyasema hayo Jumatano aliporejea katika shughuli za kisiasa, ambapo alipokea wanachama wapya waliojiunga na ODM, akiwemo aliyekuwa mwanasiasa wa Kano, Paul Sang.

Akipinga juhudi za MDG kuwavutia viongozi na wagombeaji kutoka ODM, Oburu alisema chama chake kina uzoefu mkubwa katika demokrasia ya ndani na uteuzi wa wagombeaji kutokana na historia yake ndefu ya kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *