MBADI: SITAGOMBEA KITI CHOCHOTE UCHAGUZI WA 2027
Waziri wa Hazina, John Mbadi, amesema hatagombea nafasi yoyote ya kisiasa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, akieleza kuwa mpango wake wa sasa ni kuendelea kuhudumu serikalini.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja humu nchini, Mbadi alisema hana mipango ya kurejea katika siasa za uchaguzi, bali analenga kubaki katika Baraza la Mawaziri hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Aidha, amesema ana matumaini kuwa Rais William Ruto atamteua kuendelea kuhudumu serikalini iwapo atashinda muhula wa pili wa uongozi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

