KCB RFC NDIO MABINGWA WA IMPALA FLOODLIT
Nahodha wa KCB RFC Winston Macharia amesema ushindi wa mashindano ya Impala Floodlit ya mwaka 2026 umeipa timu hiyo ari mpya inapojitayarisha kwa msimu ujao wa Kenya Cup
KCB ilitwaa taji hilo kwa mara ya kumi na moja, baada ya kuilaza Kenya Harlequins kwa alama 47 kwa 7 katika fainali iliyochezwa Jumamosi katika uwanja wa Impala, na kumaliza kusubiri kwa miaka miwili
Macharia amesema ushindi huo umetokana na umoja, bidii na kujituma kwa wachezaji, akisema umeimarisha imani yao na kuwapa motisha ya kuingia katika kampeni mpya ya Kenya Cup.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

