Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

ELDORET KUANDAA SHEREHE ZA MASHUJAA ZA MWAKA HUU

Rais William Ruto ametangaza kuwa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa mwaka huu yataandaliwa kwa ushirikiano wa kaunti za Elgeyo Marakwet, Uasin Gishu na Nandi, huku yakifanyika katika jiji la Eldoret.

Rais ametoa tangazo hilo baada ya kukutana na viongozi kutoka kaunti hizo tatu kujadili maandalizi ya hafla hiyo ya kitaifa inayotarajiwa kuwakutanisha viongozi na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

Ruto amesema maadhimisho hayo yataunganisha kaunti hizo katika maandalizi na utekelezaji wa hafla hiyo, akitoa wito kwa viongozi kuhakikisha mchakato wa maandalizi unakuwa shirikishi na wenye mafanikio.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *