CHAMA CHA UDA CHAKANUSHA MADAI YA KUPANGA KUIBA KURA OLKALAU
Chama cha UDA chake Rais William Ruto kimekanusha madai ya chama cha DCP chake aliyekuwa naibu Rais Rigadhi Gachagua kwamba kinapanga kuiba kura katika uchaguzi mdogo wa Olkalau kikisema tuhuma hizo hazina ushaihidi.
Kupitia kwa katibu Mkuu Hassan Omar UDA pia imepanga madai ya kuwapo kwa mkutano wa siri mjini Gil gil uliodaiwa kupanga njama ya wizi wa kura na kusisistiza kuwa uchaguzi wa kesho kule Olkalau utafanyika kwa haki.
Wakati huo huo tume ya uchaguzi ya IEBC imekanusha madai kuwa inaegemea upande wa serikali ikiahidi kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 kwa uwazi bila upendeleo huku kamishna wa IEBC Alutalala Mukhwana akiwaonya viongozi wa serikali na wanasiasa dhidi ya kufika katika vituo vya kupigia kura bila idhini rasmi na kusema tume ya sasa haifai kuvishwa makosa ya awali.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

