Tuesday, July 28, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

SIMON KOECH AJIPANGA KWA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA

Mshindi wa medali ya shaba katika mbio za kuruka viunzi na maji za mita 3,000 kwenye Mashindano ya Dunia kwa wanariadha walio chini ya miaka 20 mwaka 2021, Simon Koech, amesema ushindi wake katika Diamond League ya Monaco umempa ari kuelekea Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayoanza wiki ijayo mjini Glasgow, Scotland.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 22 alitwaa ushindi wake wa kwanza wa Diamond League msimu huu baada ya kutumia dakika 8:03.35, akisema alilazimika kujituma licha ya hali ya joto kali iliyokuwepo Monaco.

Koech amekiri kuwa sehemu za mwisho za mbio zilikuwa ngumu kutokana na uchovu, lakini amesema ushindi huo umempa imani kubwa anapojiandaa kuiwakilisha Kenya katika mashindano yajayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *