Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MASHINDANO YA SHULE ZA UPILI NGAZI ZA MKOA  KUENDELEA WIKI HII

Mashindano ya muhula wa pili ya Shule za Sekondari Kenya (KSSSA) Yameanza katika mikoa kadhaa yakiwakutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini kuwania ubingwa katika michezo tofauti.

Mashindano yataanza kwa ngazi za mikoa katika maeneo yote nane ya nchi kabla ya fainali za kitaifa zitakazofanyika katika MPESA Academy kuanzia Julai 28 hadi Agosti Mosi.

Wakati huo huo, Benki ya KCB imetenga shilingi milioni 20 kudhamini mashindano hayo, fedha zitakazotumika kununua vifaa vya michezo, zawadi na kuendesha shughuli mbalimbali za mashindano.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *