VIONGOZI WA SERIKALI WAMRAI KALONZO KUJIUNGA NA SERIKALI
Baadhi ya viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza wamemtaka kiongozi wa chama cha Wiper Democratic Movement Kalonzo Musyoka kujiunga na serikali.
Viongozi hao wamesema ushirikiano wa kisiasa unaweza kusaidia kuimarisha umoja wa kitaifa na kuharakisha utekelezaji wa ajenda za maendeleo nchini.
Hata hivyo, Kalonzo ameendelea kusisitiza msimamo wake wa kuendelea kuwa upande wa upinzani, akisema atashirikiana na viongozi wengine wa muungano wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

