ABUD OMAR AREJEA TUSKER FC BAADA YA MIAKA 11
Beki wa Harambee Stars, Abud Omar, amerejea rasmi Katika klabu ya Tusker baada ya miaka 11 tangu aondoke klabuni humo, kufuatia kipindi cha mafanikio cha miaka mitatu akiwa na Kenya Police FC.
Kurejea kwake kunatazamwa kama hatua muhimu kwa Tusker katika kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Omar anajiunga na Tusker akiwa ametoka katika msimu bora na Kenya Police , ambapo alitwaa tuzo za Mchezaji Bora wa Msimu, Beki Bora na Bao Bora, mafanikio yanayotarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Tusker.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

