RAIS RUTO AHIMIZA USAJILI WA WAPIGAKURA ENEO LA MAGHARIBI
Rais William Ruto amewahimiza wakazi wa eneo la Magharibi mwa Kenya wenye vitambulisho vya taifa lakini ambao bado hawajajisajili kuwa wapigakura kufanya hivyo mara fursa itakapopatikana.
Akizungumza Ikulu ya Nairobi Rais amesema usajili wa wapigakura utakuwa muhimu katika uchaguzi ujao.
Aidha, amesema tayari amewapa viongozi wa eneo hilo jukumu la kuhamasisha wananchi wote wanaostahili kujisajili wakati zoezi lijalo la usajili wa wapigakura litakapoanza.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

