Saturday, July 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MESSI ASAIDIA ARGENTINA KUTINGA FAINALI KWA KUIONDOA ENGLAND

Argentina imefuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uingereza katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mjini Atlanta.

England ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Anthony Gordon, lakini Argentina ilirejea kwa mabao ya Enzo Fernández na Lautaro Martínez, yaliyotokana na pasi za Lionel Messi, na kutwaa ushindi katika dakika za mwisho.

Kwa ushindi huo, Argentina itamenyana na Uhispania katika fainali ya Jumapili ikisaka kutetea ubingwa wake, huku England ikitarajiwa kucheza dhidi ya Ufaransa kuwania nafasi ya tatu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *