Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

AMROUCHE ATAKA AFRIKA KUKUZA VIPAJI VYA NDANI

Aliyekuwa kocha wa Harambee Stars, Adel Amrouche, amezitaka nchi za Afrika kuwekeza katika ukuzaji wa vipaji vya ndani badala ya kutegemea suluhisho za muda mfupi ili kufanikiwa katika Kombe la Dunia.

Kocha huyo raia wa Algeria amesema matokeo duni ya timu nyingi za Afrika yanatokana na kupuuzwa kwa maendeleo ya soka la vijana na mifumo ya msingi ya mchezo.

Amrouche amesisitiza kuwa mafanikio ya kudumu yatapatikana kupitia mipango ya muda mrefu, uvumilivu na uwekezaji katika kukuza wachezaji chipukizi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *