SERIKALI YAHAKIKISHIA WAKENYA UPATIKANAJI WA MAFUTA
Serikali imewahakikishia Wakenya kuwa upatikanaji wa mafuta nchini unaendelea kuwa wa kutosha licha ya mvutano unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati.
Katika taarifa yake, Waziri wa Nishati na Petroli Opiyo Wandayi amesema hali ya usafirishaji wa mafuta duniani imeathiriwa na mzozo unaozunguka Mlango wa Hormuz, lakini usambazaji wa mafuta nchini Kenya haujakatizwa.
Wandayi amesema shehena zote za mafuta zimeendelea kuwasili kwa wakati kupitia mpango wa serikali wa uagizaji wa mafuta kati ya serikali na serikali (G2G), hatua ambayo imechangia kudumisha utulivu wa bei na upatikanaji wa mafuta nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

