Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

ELOG YAIBUA WASIWASI KABLA YA UCHAGUZI WA OL KALOU

Kundi la Waangalizi wa Uchaguzi (ELOG) limeeleza wasiwasi kuhusu madai ya ukiukaji wa sheria za uchaguzi kabla ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou.

ELOG imesema waangalizi wake wameripoti visa vinavyodaiwa vya hongo kwa wapigakura, ununuzi wa vitambulisho vya taifa, kuvurugwa kwa kampeni na vurugu za kisiasa, hali inayodaiwa kuathiri mazingira ya uchaguzi.

Aidha, kundi hilo limeitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutathmini hali iliyopo na kuamua iwapo uchaguzi huo unapaswa kuendelea kama ulivyopangwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *