WAMATANGI APINGA WITO WA KUGAWA KAUNTI YA KIAMBU
Gavana wa Kaunti ya Kiambu, Kimani Wamatangi, amepinga wito wa baadhi ya viongozi wa kisiasa wa kutaka Kaunti ya Kiambu itenganishwe na eneo la Mlima Kenya au igawanywe kuwa kaunti mbili.
Wamatangi amesema mapendekezo hayo yana nia ya kisiasa na yanalenga kuleta mgawanyiko badala ya kuendeleza maslahi ya wananchi.
Aidha, amewataka viongozi wanaounga mkono mpango huo kueleza maendeleo waliyoyatekeleza walipokuwa madarakani, akisisitiza kuwa wakazi wa Kiambu wanahitaji huduma na maendeleo, si siasa za migawanyiko.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

