Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MAANZO AWAHIMIZA WAPIGAKURA WA OL KALOU KUDUMISHA AMANI

Seneta wa Makueni, Dan Maanzo, amewataka wapigakura wa Ol Kalou kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge bila hofu wala vitisho.

Maanzo amesema wananchi wanapaswa kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa amani na bila kushawishiwa au kutishwa na mtu yeyote.

Aidha, amewahimiza kuripoti mara moja kwa mamlaka husika jaribio lolote la kuzua vurugu au kuvuruga mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na uwazi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *