KITANY: OL KALOU SI KIPIMO CHA UMAARUFU WA RUTO NA GACHAGUA
Mbunge wa Aldai, Marianne Kitany, amesema uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou haupaswi kutazamwa kama kipimo cha mwisho cha umaarufu kati ya Rais William Ruto na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Kitany amesema baada ya chama cha UDA kushinda chaguzi ndogo za Mbeere na Malava, hoja kwamba kila uchaguzi mdogo ni kipimo cha nguvu za kisiasa imepoteza uzito.
Aidha, amesisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa Ol Kalou yanapaswa kuakisi uamuzi wa wapigakura wa eneo hilo, badala ya kutafsiriwa kama kipimo cha umaarufu wa viongozi wa kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

