AUKOT AUNGA MKONO KESI DHIDI YA MASPIKA
Kiongozi wa chama cha Third Way Alliance, Dkt. Ekuru Aukot, amesema anaunga mkono hoja ya asasi ya Vocal Africa kwamba Maspika wa Bunge wanapaswa kuepuka siasa za vyama.
Aukot amesema Spika anapoonyesha upendeleo wa kisiasa, huwa vigumu kwa mabunge kutekeleza wajibu wake wa kuiwajibisha serikali ipasavyo.
Aidha, amesisitiza kuwa viongozi wanaosimamia mabunge wanapaswa kubaki huru na wasioegemea upande wowote ili kulinda uwajibikaji na demokrasia nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

