EACC YAIDHINISHA SIKU YA KUPAMBANA NA UFISADI NCHINI
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC inaadhimisha Siku ya Afrika ya Kupambana na Ufisadi kwa kuhimiza kuimarishwa kwa uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Tume hiyo imesema maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kutathmini hatua zilizopigwa katika vita dhidi ya ufisadi na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za umma, sekta binafsi na wananchi katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa.
EACC imeeleza kuwa kuzingatia misingi ya uadilifu na uwajibikaji ni muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za umma, kuimarisha utawala bora na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

