LONGISA AJIANDAA KURITHI NAFASI YA KIPYEGON KATIKA MITA 1500
Bingwa wa mbio za mita 1,500 katika mashindano ya vyuo vikuu nchini Marekani (NCAA), Rosemary Longisa, amesema yuko tayari kuendeleza ubora wa Kenya katika mbio hizo baada ya Faith Kipyegon kuelekeza nguvu zake kwenye mbio za masafa marefu.
Longisa amesema anaamini wakati umefika kwa kizazi kipya cha wanariadha kuchukua jukumu la kuiwakilisha Kenya katika mbio za mita 1,500 kwenye jukwaa la kimataifa.
Hatua hiyo inajiri baada ya Kipyegon kuashiria kuwa atabadilisha mwelekeo wa taaluma yake, hatua inayotarajiwa kufunga ukurasa wa mafanikio makubwa aliyoyapata katika mbio hizo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

