Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

PORTUGAL YAFUZU HATUA YA 16 BORA KWA BAO LA DAKIKA ZA MWISHO

Ureno imefuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Croatia mabao 2-1 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali.

Mshambuliaji aliyeingia kipindi cha pili, Gonçalo Ramos, aliifungia Ureno bao la ushindi katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Rafael Leão.

Croatia, iliyotengeneza nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo, ilidhani imesawazisha katika sekunde za mwisho, lakini bao la Joško Gvardiol lilikataliwa kutokana na kuotea.

Ushindi huo umeihakikishia Ureno nafasi katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *