Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MATIANG’I AONYA KUHUSU USALAMA WA TAIFA KISA ONGEZEKO LA WAHUNI

Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt. Fred Matiang’i, ameonya kuwa Kenya inaelekea katika hali ya machafuko kutokana na kuongezeka kwa vurugu za kisiasa, visa vya utekaji nyara na matumizi ya makundi yenye silaha kuwashambulia wakosoaji wa serikali.

Matiang’i amelaani tukio la Keumbu, Kisii, ambapo washiriki wa mkutano wa kisiasa walirushiwa mawe mbele ya maafisa wa polisi waliokuwa eneo hilo, akisema matukio hayo yanaibua wasiwasi kuhusu usalama wa wananchi.

Amesema kuvurugwa kwa mikutano ya amani na kuendelea kwa vitendo vya kutoadhibiwa kwa wahusika ni ishara kwamba mamlaka ya sheria yanazidi kudhoofika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *