Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RAIS RUTO AWAJIBU WAKOSOAJI WAKE KUHUSU KUKARABATI IKULU

Rais William Ruto amewajibu wakosoaji wake  kuhusu ukarabati unaoendelea katika Ikulu, akisema Ikulu si mali yake binafsi wala ofisi yake ya kibinafsi, bali ni taasisi ya taifa inayopaswa kutunzwa kwa manufaa ya viongozi wa sasa na wa baadaye.

Akizungumza hii leo katika Ikulu ya Nairobi Rais amesema ukarabati unaofanyika unalenga kuhifadhi hadhi ya makao rasmi ya Rais na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi pamoja na kupokea wageni wa kitaifa na kimataifa.

Pia amesisitiza kuwa ukarabati huo ni uwekezaji katika mali ya umma na si kwa manufaa yake binafsi.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *