Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

SHABANA WAMNASA KIPA BIXENTE OTIENO

Klabu ya Shabana imeimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya FKF baada ya kumsajili kipa Bixente Otieno kwa uhamisho wa bure kutoka Posta Rangers.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 ametia saini mkataba wa muda mrefu baada ya mkataba wake na Posta Rangers kumalizika, akimaliza uvumi uliokuwa ukimhusisha na klabu mbalimbali.

Usajili huo unalenga kuimarisha safu ya ulinzi ya Shabana chini ya kocha mpya Ahmed Fathi, ambaye anasisitiza nidhamu ya kujilinda na matumizi bora ya makipa katika ujenzi wa mashambulizi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *