NPS: HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA
Msemaji wa Huduma ya Taifa ya Polisi, Michael Muchiri, amesema Inspekta Jenerali wa Polisi ameahidi kuongoza mapambano dhidi ya uhalifu bila ubaguzi.
Muchiri amesema yeyote atakayehusika na vitendo vya uhalifu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, bila kujali cheo au nafasi yake katika jamii.
Kuhusu mbunge anayetajwa katika uchunguzi unaoendelea wa vurugu zilizotokea katika eneo la Keumbu kaunti ya Kisii, Muchiri amesema Mbunge huyo anapaswa kupewa nafasi ya kujibu tuhuma zinazomkabili huku akiwataka wananchi kuziachia mamlaka za uchunguzi kufanya kazi yao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

