MAMLAKA YA KRA YASITISHA KUTOZA USHURU MAJI YA KUNYWA YALIYO KWENYE CHUPA
Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA imetangaza kuwa maji ya kunywa yaliyowekwa kwenye chupa yanayotengenezwa au kuingizwa nchini hayatatozwa tena ushuru wa bidhaa kufuatia mabadiliko yaliyoletwa kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2026.
Kupitia taarifa kwa umma , KRA imesema kuwa mabadiliko hayo yalianza kutekelezwa rasmi Julai 1, 2026, baada ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2026 kufanya marekebisho kwenye Jedwali la Kwanza la Sheria ya Ushuru wa Bidhaa.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

