Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA GHASIA ZA KISIASA KISUMU

Mtu mmoja amefariki dunia, wengine kadhaa kujeruhiwa na pikipiki tisa kuteketezwa baada ya makundi hasimu ya vijana kupigana nje ya Kanisa la St. Stephen’s mjini Kisumu.

Ghasia hizo zilizuka baada ya kundi moja kudaiwa kujaribu kuvamia kanisa ambako Gavana wa Siaya James Orengo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna walikuwa wakihudhuria ibada, lakini likazuiwa na kundi jingine.

Baada ya tukio hilo, Orengo na Sifuna wameisuta serikali wakidai kuwa imelegeza udhibiti wa vurugu za kisiasa, huku wakionya dhidi ya kuongezeka kwa matukio ya ukosefu wa usalama nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *