OBURU: ODM HAITASIMAMISHA MGOMBEA URAIS 2027
Kiongozi wa ODM, Oburu Odinga, amesema chama hicho hakitasimamisha mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Badala yake, amesema ODM itaunga mkono azma ya Rais William Ruto kutetea kiti chake kwa muhula wa pili, hatua anayosema inalenga kuimarisha serikali jumuishi na kuharakisha maendeleo katika eneo la Nyanza.
Kauli hiyo imeungwa mkono na Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga, ambaye amesema Nyanza imenufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya ushirikiano wa kisiasa uliopo sasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

