MOTO WATEKETEZA BWENI LA SHULE YA HOBUNAKA KAUNTI YA VIHIGA
Zaidi ya wanafunzi 100 wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Hobunaka katika Kaunti ya Vihiga wamekosa mahali pa kulala baada ya moto kuteketeza bweni moja usiku wa Jumanne.
Moto huo uliteketeza mali ya thamani ya mamilioni ya shilingi, huku wanafunzi na wakazi wa eneo hilo wakijaribu kuuzima kwa kutumia ndoo za maji.
Taarifa za awali zinadai kuwa baadhi ya wanafunzi waliteketeza bweni hilo baada ya kunyimwa ruhusa ya kutazama mechi ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Misri, ingawa uongozi wa shule haujathibitisha madai hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

