Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MAHAKAMA YAMWACHILIA HURU BOB NJAGI, YAFUNGA FAILI LA KESI

Mahakama ya Hakimu mjini Kajiado imemwachilia huru mwanaharakati Bob Njagi na kuamuru jalada la kesi dhidi yake lifungwe.

Njagi alikamatwa Juni 24, siku moja kabla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa maandamano ya Gen Z. Mkuu wa DCI Kitengela, Eric Ambasa, aliiambia mahakama kuwa uchunguzi ulikuwa ukiendelea kuhusu madai ya uhaini, lakini hakuna mashtaka yaliyokuwa yameidhinishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP).

Njagi, aliyewakilishwa na mawakili sita akiwemo Gavana wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, alidai kuwa kukamatwa na kuzuiliwa kwake kulikiuka haki zake za kikatiba.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *