WANJIGI: HOFU ILIPUNGUZA IDADI YA WATU KWENYE MAANDAMANO
Kiongozi wa chama cha Safina, Jimi Wanjigi, amesema hali ya hofu na hatua kali za usalama zilichangia kupungua kwa idadi ya waliojitokeza katika maandamano ya Saba Saba.
Akizungumzia maadhimisho hayo, Wanjigi amesema wananchi wengi walichagua njia mbadala za kueleza kutoridhishwa kwao badala ya kushiriki maandamano ya mitaani.
Aidha, amedai kuwa hatua za polisi za kuzuia maandamano zilichangia idadi ndogo ya washiriki katika miji ya Nairobi na Mombasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

