MAHAKAMA YASITISHA UENDESHAJI WA KITUO CHA EBOLA LAIKIPIA
Mahakama Kuu imesitisha Wizara ya Afya kuanza kuendesha kituo kinachohusishwa na Ebola katika kambi ya kijeshi ya Laikipia, hadi serikali itakapowasilisha nyaraka muhimu zinazoeleza jinsi kituo hicho kilivyoanzishwa na hatua za usalama zilizowekwa.
Jaji Patricia Mande amesema wizara ilikiuka misingi ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa umma kwa kuficha taarifa muhimu kutoka kwa wakazi na serikali ya kaunti ya Laikipia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

