ARSENAL KUIKABILI MANCHESTER CITY KATIKA MECHI ZA LIGI KUU
Ligi Kuu ya Uingereza inaendelea leo kwa mechi moja, Nottingham Forest ikiikaribisha Chelsea kuanzia saa tano usiku, kabla ya mechi nyingine kuendelea kesho.
Kesho, Manchester United itamenyana na Brentford saa kumi na mbili jioni, Leeds ikiikaribisha Coventry kwa wakati huo huo, huku Ipswich Town ikivaana na Aston Villa saa mbili na nusu usiku.
Jumapili, Everton itakutana na Liverpool saa tisa alasiri, huku Brighton, Fulham, Sunderland na Crystal Palace zikiwa na mechi kuanzia saa kumi na moja, kabla ya Arsenal kuikaribisha Manchester City saa moja na nusu usiku.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

